Kwa mujibu wa ripoti ya kikundi cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, amewapokea mazuwari wa Arubaini wa Nigeria, na katika hotuba yake iliyosadifiana na tarehe 8 mwezi wa Safar, alisisitiza umuhimu wa matembezi ya Arubaini na kusema kuwa mkusanyiko huu mkubwa katika njia ya Najaf kuelekea Karbala ni matokeo ya mafundisho ya Imam Husein (as) na Ahlul-Bayt (as).
Aidha, alizungumzia kuhusu tukio la Karbala na kusema: Uadui kati ya Bani Umayyah, Yazid na wafuasi wao haujawahi kupunguza hata chembe ya mapenzi ya Ahlul-Bayt (as) katika nyoyo za Mashia na wapenzi wao.
Baadhi ya washiriki waliokuwa wakifuatilia kwa karibu Hotuba ya Sheikh Zakzaky
Sheikh Zakzaky alisema: Wale wanaotekeleza mauaji ya kimbari katika historia watalaaniwa milele, kuanzia Firauni aliyefanya kitendo hiki kibaya katika zama za kale, hadi kwa wahalifu wa leo.
Mwishoni, kiongozi wa Harakati ya Kiislamu aliuombea dua msafara huo kwa kusema: Inshaallah, Mwenyezi Mungu Mtukufu aufanye msafara huu wa mazuwari uwe salama.
Chanzo: Tovuti rasmi ya Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.
Maoni yako